RIPOTI: SHERYL ADHIAMBO ALIFARIKI KWA JERAHA LA RISASI
Uchunguzi wa maiti umebaini kuwa Sheryl Adhiambo, mwanafunzi wa miaka 21 wa Chuo cha Mafunzo ya Madaktari cha Kenya (KMTC), alifariki dunia kutokana na jeraha moja la risasi kichwani.
Uchunguzi huo, uliofanywa na wanapatholojia Grace Midigo na Simon Omuok, uligundua kuwa risasi iliingia upande wa kushoto wa kichwa chake na kutoka nyuma, na kusababisha kupasuka kwa cavity ya ubongo.
Madaktari hao wamesema kuwa jeraha hilo lilikuwa baya mno na hangeweza kunusurika, na hivyo kuonyesha kuwa kifo chake kilikuwa cha ghafla na cha hatari.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































