MAGENDO YA KAHAWA SIRISIA
Serikali inapoteza mamilioni ya pesa za ushuru kufuatia ongezeko la biashara za magendo ya kahawa kutokana na utepetevu wa maafisa wa upelelezi DCI katika eneo la Sirisia kaunti ya Bungoma ambao wamehishindwa kuwanasa wahusika.
Ni kauli ya mbunge wa eneo hilo John Waluke, akidai maafisa hao wanajihusisha kwenye magendo hayo na wafanyabiashara katika taifa jirani la Uganda.
Ameitaka tume ya maadili na kukabili ufisadi EACC kuwachunguza na kuwachukulia hatua maafisa hao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































