#Football #Sports

KOCHA AFICHUA SABABU YA KUMWACHA NJE OLUNGA

Naibu meneja wa timu ya taifa Harambee Stars Vasili Manousakis ameweka wazi sababu za kumwacha nje ya kikosi nahodha wa timu hiyo Michael Olunga wanapojiandaa kwa mechi za kirafiki wiki hii.

Kulingana na Manousakis, lengo ni kuwaondolea shinikizo baadhi ya wachezaji wa timu hiyo akiwemo Olunga, na kupisha fursa kwa wachezaji wengine, kinyume na ripoti mitandaoni kwamba uamuzi huo ulikuwa wa kinidhamu.

Stars wataanza mechi yao ya kirafiki dhidi ya Equatorial Guuinea Ijumaa wiki hii kabla ya Senegal tarehe 18 mwezi huu, mech izote zikiratibiwa kuchezwa nchini Uturuki.

Mbali na Olunga, wachezaji wengine muhimu wameachwa nje, Manousakis akisema baadhi yao wana majeraha madogo madogo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KOCHA AFICHUA SABABU YA KUMWACHA NJE OLUNGA

JORGE FRUTOS KUJAZA PENGO LA YAMAL “LA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *