EACC: UFISADI UNAZIMA NDOTO ZA VIJANA NCHINI
Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi, EACC, imetoa onyo kwamba ufisadi unaathiri kwa kiwango kikubwa vijana nchini, ikisema athari zake zinapunguza fursa muhimu za maendeleo kwa kizazi hicho.
Takwimu mpya zinaonyesha kuwa utoaji hongo na matumizi mabaya ya fedha za umma vinaendelea kudhoofisha nafasi za elimu, ajira na mifumo ya usaidizi wa kifedha, hali inayodaiwa kuwazuia vijana kufikia uwezo wao kamili.
Mkurugenzi Mkuu wa EACC, Abdi Mohamud, amesema ripoti ya utafiti wa kitaifa kuhusu maadili na ufisadi iliyofanywa na tume hiyo imebaini kuwa ufisadi ni shambulio la moja kwa moja linalowakumba vijana kila siku na kuharibu ndoto zao.
Imetayarishwa na Cyrus SIfuna
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































