NAIBU GAVANA WA HOMA BAY AJIUZULU
Kinyang’anyiro kikali kinatarajiwa kwenye uchaguzi wa ugavana kaunti ya Homa Bay katika uchaguzi mkuu ujao kufuatia kujiuzulu kwa naibu gavana, Joseph Magwanga, aliyeaminika kuwa na ushawishi mkubwa kisiasa kwenye uchaguzi mkuu uliopita kabla yake kushawishiwa kumuunga mkono gavana wa sasa Gladys Wanga.
Katika taarifa, Magwanga ambaye hajakuwa akielewana kisiasa na Wanga, amesema uamuzi huo umejiri kufuatia mashauriano na viongozi, wafuasi na familia yake, akidai kuzuiwa kuingia afisini mwake tangu Desemba mwaka jana.
Uamuzi wake unajiri baada ya kutangaza kuwania ugavana kwenye uchaguzi mkuu ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































