RATIBA YA KENYA CUP VOLLEYBALL YATOLEWA
Shirikisho la mchezo wa Voloboli KVF limethibitisha kwamba toleo la pili la ubingwa wa Kenya Cup Volleyball litaandaliwa kuanzia tarehe 15 hadi tarehe 18 mwezi huu katika uga wa Kasarani Indoor Arena.
Tangazo linaashiria mwanzo rasmi wa kalenda ya voliboli katika msimu wa 2025-26, ambapo timu za wanaume na wanawake zitashiriki.
Aidha, shirikisho hilo limesema droo ya kutoa ratiba mechi za kipute hicho itafanyika Jumamosi hii, ambapo timu zitafahamu wapinzani wao.
Taji la Kenya Cup ambalo ni jipya, lilizinduliwa kuendeshwa sambamba na ligi ya kitaifa, ili kutoa nafasi kwa klabu kushiriki mechi nyingi na kupata kupata ufahamu na ushindani mbali na kutoa nafasi kwa ukuzaji wa vipaji.
Kenya Cup ilizinduliwa Januari mwaka jana na kutamatika Julai mwaka huo, mabingwa wakiwa KCB Women’s Volleyball Team na GSU kwa wanaume.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































