REGRAGUI AKOSOA VIKALI FUJO KATIKA FAINALI YA AFCON
Kocha wa Morocco, Walid Regragui, amekosoa vikali tukio alilolitaja kuwa la “aibu” lililotokea katika fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika, baada ya wachezaji wa Senegal kuondoka uwanjani kwa kupinga uamuzi wa waamuzi kabla ya kurejea na kushinda mchezo huo katika muda wa nyongeza.
Akizungumza baada ya Morocco kupoteza fainali hiyo 1-0 jijini Rabat, Regragui alisema tukio hilo lilitoa taswira mbaya ya soka la Afrika mbele ya dunia.
Regragui aliongeza kuwa kusimamishwa kwa mchezo kwa zaidi ya dakika 10 huku dunia ikishuhudia si jambo la kuvutia kwa mashindano ya hadhi ya AFCON.
Morocco walikuwa na nafasi ya dhahabu ya kushinda taji hilo walipopewa penalti katika dakika za majeruhi za mwisho wa muda wa kawaida, huku mchezo ukiwa bado bila bao.
Mwamuzi kutoka DR Congo, Jean-Jacques Ndala, alitoa penalti hiyo baada ya kurejea VAR kufuatia mkwaju wa beki wa Senegal, El Hadji Malick Diouf, dhidi ya Brahim Diaz.
Hata hivyo, mchezo ulisimamishwa kwa takriban dakika 20 kabla ya Diaz kupiga penalti, ambayo alipiga kwa mtindo wa Panenka lakini ikadakwa kwa urahisi na kipa.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































