#Business

NSSF KUWEKEZA KSH 30B KATIKA BARABARA YA RIRONI–MAU SUMMIT

Hazina ya kitaifa ya hifadhi ya jamii, NSSF, imetangaza mkakati mpya wa uwekezaji utakaoelekeza michango ya pensheni ya wafanyakazi katika maendeleo makubwa ya miundombinu na majengo, unaolenga kuongeza mapato na kuwezesha malipo ya haraka kwa wanachama.

Hatua hiyo inalingana na lengo la hazina ya kutoa asilimia 17 ya mapato ya kila mwaka huku ikijitahidi kukuza msingi wake wa mali hadi Ksh1 trilioni. Chini ya mkakati wake wa uwekezaji, NSSF inapima ahadi ya hadi Ksh30 bilioni kwa barabara inayopendekezwa ya Rironi–Mau Summit. Mike Macharia, mdhamini anayewakilisha Shirikisho la Waajiri nchini (FKE), amesema mradi huo unatarajiwa kuleta mapato dhabiti huku ukisaidia kupunguza msongamano kwenye Barabara Kuu ya Nakuru inayotumika sana.

Macharia aidha ameeleza kuwa mwanzo barabara hiyo itatumika na wananchi wanaolipia huduma za barabara  ili kuwezesha mfuko huo kurejesha uwekezaji wake, na kuongeza kuwa madereva ambao hawapendi kulipa bado watapata njia mbadala isiyo ya kulipia.

Imetayarishwa na Maurine Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *