TANZANIA YAHARAMISHA MAANDAMANO
Serikali ya Tanzania imewekwa kwenye darubini ya ulimwengu kuona jinsi itakavyowakabili waandamanaji baada ya kupiga marufuku maandamano ya leo huku taifa hilo likiadhimisha siku ya Uhuru.
Maandamano hayo yaliyopangwa na viongozi wa upinzani, yalilenga kupinga uongozi wa taifa hilo na madai ya kufeli kwa serikali, ila vitengo vya usalama vikayataja kuwa jaribio la kuipindua serikali na kuwataka wananchi wote wasio watoaji wa huduma za dharura kusalia nyumbani hii leo.
Hata hivyo, wanaharakati kutoka Afrika Mashariki wameitaka serikali hiyo kuheshimu haki za kiraia.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































