PVK YAKOSOA SERA TATA YA MAKANISA
Muungano wa Pentecostal Voice of Kenya PVK umeitaka serikali kusitisha mchakato wa kubuniwa kwa sera ya kudhibiti mashirika ya kidini, kufuatia kuondolewa kwa mswada wa kudhibiti mashirika hayo wa mwaka 2024.
Ikiongozwa na mwenyekiti wake Apostle Peter Manyuru ambaye pia ni kiongozi wa kanisa la JTM, PVK imehofia kwamba sera hiyo itayanyima makanisa na mashirika yasiyokuwa ya kiserikali uhuru wa kujieleza.
Amesisitiza kuwa serikali haikuyahusisha makanisa kwenye kubuniwa kwa sera hiyo.
Wamemtaka Rais William Ruto kutimiza ahadi yake ya kutetea uhuru wa makanisa.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































