ODM:TUNGALA IMARA NA MAARUFU
Uongozi wa chama cha ODM umesisitiza kuwa chama hicho kingali imara kutokana na ushindi wake wa viti vya ubunge kwenye uchaguzi mdogo wa hapo jana, ukisema chama hicho kitaunda serikali baada ya uchaguzi mkuu ujao.
Wakiongozwa na naibu kinara wa chama hicho Abdulswamad Nassir na mwenyekiti wa kitaifa Gladys Wanga, ODM imehusisha ushindi huo pia na ushirikiano wa kisiasa na Rais William Ruto.
Chama hicho kimedumisha viti vyake katika maeneo bunge yote 3 ambayo ni Ugunja, Kasipul na Magarini.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 




















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































