UPINZANI: SERIKALI INAPANGA KUVURUGA UCHAGUZI MAGARINI
Viongozi wa muungano wa upinzani wameibua madai kwamba serikali inapanga kuvuruga uchaguzi mdogo katika eneo bunge la Magarini kaunti ya Kilifi na kuhitilafiana na zoezi hilo ikiwemo kuwasafirisha wapiga kura kutoka nje ya Magarini.
Kulingana na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka na mwenzake wa DAP-K Eugene Wamalwa, wizi wa kura uliofanyika kwenye uchaguzi wa mwaka wa 2022 eneo hilo jinsi ilivyobainika mahakamani, unaweza kujirudia iwapo Wakazi hawatakuwa macho.
Upinzani unampigia debe mwaniaji wa DCP Stanley Karisa huku ODM na PAA zikimpigia debe Harrison Kombe.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































