DROO YA UEFA KUELEKEA KOMBE LA DUNIA YAKAMILIKA
Mabingwa mara 4 wa kombe la dunia Italia, watakabiliana na North Macedonia katika kusaka tiketi ya kushiriki kombe la dunia mwaka ujao kupitia mwondoano yaani playoff, baada ya kukosa tiketi ya moja kwa moja.
Kwenye droo iliyofanyika hapo jana jijini Zurich, iwapo Italia watashinda mechi hiyo ya tarehe 26 mwezi Machi mwaka ujao, watamenyana na mshindi kati ya Wales na Bosnia-Herzegovina siku 5 baadaye.
Italia watalenga kuepuka aibu ya kunyimwa fursa ya kushiriki dimba hilo kwa mara ya 3 mfululizo, baada ya kuondolewa na Sweden mwaka 2018 na North Macedonia mwaka 2022.
Katika mechi nyingine, Ukraine wataweka kando masaibu ya vita nyumbani kwao watakapomenyana Sweden inayojumuisha nyota kama vile Viktor Gyokeres wa Arsenal na mwenzake wa Liverpool Alexander Isak.
Mshindi wa pambano hilo atamenyana na mshindi kati ya Poland na Albania
Jamhuri ya Ireland nayo itachuana na Czech Republic, mshindi kati yao akiwa mwenyeji wa mshindi kati ya Denmark na North Macedonia.
Uturuki watakabana koo na Romenia waliowashangaza wengi walipofika robo fainali ya dimba hilo mwaka 1994 nchini Marekani
Mshindi kati yao atamenyana na Slovakia au Kosovo, wanaolenga tiketi ya kushiriki dimba hilo kwa mara .
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































