WADAU WAONYWA DHIDI YA WIZI WA MTIHANI
Washikadau katika zoezi la mtihani wa kidato cha 4 KCSE unaoendelea wametakiwa kujiepusha na visa vya udanganyifu ili kudumisha uadilifu wa mtihani huo.
Akizungumza baada ya kuongoza zoezi la ufunguzi wa kasha la mitihani hiyo katika eneo bunge la Webuye East, kamishna wa baraza la mitihani wa kitaifa KNEC Zephaniah Koech ameonya kuwa hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi ya watakaopatikana wakivunja kanuni za mtihani.
Naye naibu kamishna wa eneo hilo Joyce Nyabonyi akitoa hakikisho kuhusu usalama wakati na hata baada ya mtihani huo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































