RUTH ODINGA ATAKA LINDA GROUND NA LINDA MWANANCHI KUVUNJWA
Mwakilishi wa Wanawake wa Kaunti ya Kisumu, Ruth Odinga, ametoa wito wa kuvunjwa au kuunganishwa kwa makundi ya Linda Ground na Linda Mwananchi ndani ya chama cha ODM, akisisitiza umuhimu wa umoja wa chama hicho.
Katika taarifa aliyochapisha kwenye mitandao yake ya kijamii Jumatatu, Odinga ambaye pia ni katibu wa maandalizi wa chama hicho, amesema makundi hayo mawili yamekuwa yakitawala mjadala ndani ya chama katika siku za hivi karibuni huku yakishindana kila moja kuonyesha ushawishi wake.
Aidha, ameeleza kuwa ili chama kiwe na nguvu ya kujadiliana kuelekea uchaguzi mkuu wa 2027, ni lazima kiwasilishe timu moja iliyoungana itakayoongeza nafasi yake katika mazungumzo ya kabla ya muungano.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































