#Rugby #Sports

KCB YAKWEPA KIKAANGO CHA MENENGAI OILERS

Timu ya KCB RFC ilionyesha ukakamavu katika kipindi cha pili na kujiondoa kwenye kikaango cha Menengai, baada ya kuwazaba wanamafuta hao 25-15 katika kipute cha Kenya Cup ugani ASK Showgrounds.
Menengai walitangaza hatari mapema ila wakabaki wakijilaumu kwa nafasi walizopoteza ikiwemo penalti ambayo huenda ingewapa uongozi.
KCB walitumia fursa hiyo kuwakaanga kwa mafuta yao, Nick Okullo akivuka na kuwapa trai ya kwanza, Brian Wahinya akiongeza za ziada kufanya mambo kuwa 7-0.
Licha ya juhudi za Menengai Oilers, KCB walikaa ngumu na kuhakikisha mambo yanaishia 25-15.
Kwa sasa KCB wameelekeza makini yao kwa pambano dhidi ya Kabras RFC Jumamosi wiki hii.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KCB YAKWEPA KIKAANGO CHA MENENGAI OILERS

INGWE YAWARARUA GLAMOUR BOYS

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *