SIKU KUBWA UGANDA
Mamilioni ya raia nchini Uganda wameratibiwa kushiriki uchaguzi mkuu hii leo huku viongozi wa upinzani na wanaharakati wakiibua madai ya uwepo wa njama ya udanganyifu kwenye uchaguzi huo hasa kutokana na na kuzimwa kwa mitandao ya mawasiliano.
Rais Yoweri Museveni analenga kuendeleza utawala wake wa zaidi ya miaka 40 anapomenyana na mpinzani wake Robert Kyagulanyi maarufu kama Bobi Wine kwenye uchaguzi huo.
Kulingana na upinzani, njama ya wizi inapangwa kutumiwa kwenye vifaa vya kielektroniki vya kupiga kura.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































