TAHARUKI YAJITOKEZA CBD NAIROBI
Taharuki imeshuhudiwa katika eneo la biashara katikati ya jiji la Nairobi, CBD, baada ya polisi kuingilia kati maandamano ya wahudumu wa magari ya uchukuzi wa umma.
Maafisa wa polisi wameonekana wakiondoa vizuizi barabarani na kung’oa nambari za magari ya matatu yaliyokuwa yameegeshwa katika barabara kuu, huku wakijaribu kurejesha hali ya kawaida ya usafiri jijini.
Maandamano hayo ni sehemu ya malalamishi ya wahudumu wa matatu wanaodai serikali imeshindwa kuwalinda dhidi ya mashambulizi ya umati, hasa visa ambapo waendesha boda boda huharibu au kuchoma matatu kufuatia ajali za barabarani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































