WAVUNJAJI WA SHERIA ZA MITIHANI WANASWA
Jumla ya watu 36 waliokamatwa kuhusiana na visa vya udanganyifu wa mitihani unaoendelea wa KCSE wanatarajiwa kufikishwa mahakamani hii leo kufunguliwa mashtaka ya ukiukaji wa mwongozo wa mitihani ya kitaifa.
Miongoni mwa waliokamatwa ni wanafunzi wa vyuo vikuu 3 waliokauwa wakiwafanyia wanafunzi mitihani katika kaunti ya Nairobi na Kericho, wengine wakiwa watahiniwa waliopatikana na simu, wasimamizi wa vituo vya mtihani huo na walimu.
Wizara ya elimu imesema uchunguzi zaidi unaendelea na kwamba wahusika watakabiliwa kisheria.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































