KINDIKI: NYOTA KUWAFIKIA MILIONI 2
Mradi wa ujasiriamali wa serikali wa NYOTA unalenga kupanuliwa ili kuwafaidi vijana zaidi ya milioni 2 kote nchini, tayari vijana 820,000 wakiwa wamelengwa
Haya ni kulingana na naibu Rais Kithure Kindiki, akisema lengo la mradi huo ni kuona vijana wengi wamepata mafunzo na mtaji wa kuendesha biashara ili kujikimu kiuchumi.
Jumla ya vijana 121,000 wamepokea ufadhili wa serikali, ambapo kila kijana alipokea shilingi 22,000 katika awamu ya kwanza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































