MLIPA USHURU KUGHARAMIA PENISHENI YA WABUNGE
Wakenya wanakabiliwa na uwezekano wa kuongezewa ushuru ili kugharamia malipo ya uzeeni ya wabunge iwapo mswada uliowasilishwa bungeni na mbunge wa Kitui Central Makali Mulu utapitishwa bungeni na kuwa sheria.
Mswada huo unalenga masuala kadhaa ikiwemo kuwapa wabunge waliohudumu kwa muhula mmoja muda zaidi wa kulipa malipo yao ya penisheni waliopokea awali, huku wale waliohudumu kwa mihula 2 au zaidi wakilindwa dhidi ya kupoteza penisheni yao ya kila mwezi iwapo watapoteza viti vyao na kisha kurejea bungeni.
Mjadala huo uliibuka mjini Naivasha, wabunge wakijadili maslahi yao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































