KENYATTA UNIVERSITY WANYAKUA TAJI LA KUSF
Kenyatta University wamejinyakulia taji la soka la wanawake la Kenya Universities Sports Federation (KUSF) wakati wa mashindano ya International Women’s Day yaliyofanyika katika viwanja vya chuo kikuu cha Taita Taveta mjini Voi.
Kenyatta University waliwashinda University of Eldoret mabao 2–0 katika fainali na kumaliza mashindano ya siku tatu bila kupoteza mchezo.
Mabao ya Sheila Juma na Hope Wandera katika kila kipindi yaliihakikishia KU ushindi huo na kurejesha taji hilo baada ya mwaka jana kumaliza katika nafasi ya pili nyuma ya Masinde Muliro University.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































