ODM YATOA MASHARTI KWA KENYA KWANZA
Chama cha ODM kimeshinikiza mazungumzo na serikali ya Kenya Kwanza kuhusu mgao wa nyadhifa kuu kabla ya uchaguzi mkuu ujao, licha ya ahadi yake ya kuiunga mkono serikali hiyo.
Kikiongozwa na naibu kinara na ambaye pia ni seneta wa Vihiga Godfrey Osotsi na kiongozi wa walio wachache bungeni Junet Mohammed, ODM imesema haitajiunga na serikali pasipo na makubaliano ya wazi.
Viongozi hao walikuwa wakizungumza katika eneo la Lugari.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































