VIONGOZI TRANS NZOIA WAHIMIZWA KUSHIRIKIANA
Baadhi ya wawakilishi wadi katika kaunti ya Trans Nzoia wamewahimiza viongozi kwenye kaunti hiyo kutoingiza siasa katika masuala ya maendeleo, wakisema mwelekeo huo utasababisha wakazi kusalia nyuma kimaendeleo.
Wakiongozwa na mwenzao wa Hospital Eric Wafula, wawakilishi wadi hao wamehimiza ushirikiano wa viongozi wa kaunti hiyo na serikali kuu kama kigezo cha maendeleo.
Wito huo unajiri baada ya Rais William Ruto kuahidi shilingi bilioni 1 kuimarisha hospitali ya level 4 ya Wamalwa Kijana mjini Kitale.
Imeatayarishwa na Antony Nyongesa
English 





























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































