ALDRINE KIBET ATAJWA KIKOSINI HARAMBEE STARS
Timu ya taifa ya soka Harambee Stars itacheza mechi mbili za
kirafiki za kimataifa mjini Antalya, Uturuki, wakati wa dirisha la
FIFA mwezi ujao, kati ya Novemba 10 hadi 18.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi iliyotolewa na Shirikisho la Soka
Nchini Stars Itavaana na Madagascar tarehe 14 Novemba, kabla
ya kukutana na Comoros.
Kocha mkuu Benni McCarthy ametangaza kikosi cha mwisho
kwa michezo hiyo, ambacho kimejumuisha mchanganyiko wa
vijana chipukizi na wachezaji wazoefu wanaorejea.
Miongoni mwa nyota waliovutia macho ni Aldrine Kibet,
anayesakata soka katika klabu ya Celta Vigo nchini Uhispania,
ambaye ameitwa kwa mara ya kwanza katika timu ya wakubwa
kutokana na ubunifu na utulivu wake uwanjani.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































