WANAHARAKATI BUSIA WASHINIKIZA HAKI KWA MWANAMME
Mwanamme mwenye umri wa miaka 25 mjini Busia anaendelea kuuguza majeraha hospitalini baada ya kudaiwa kumwagiwa maji ya moto na mkewe, huku familia ikiikosoa mahakama kwa madai ya kuharakisha kumwachia kwa dhamana mshukiwa.
Kulingana na Ishmael Oundo, tukio hilo lilisababishwa na ugomvi kati yake na mkewe, wakazi na wanaharakati wakishinikiza mshukiwa akamatwe upya.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































