KIPKORIR ALENGA KUVUNJA REKODI YA SEKUNDE 43
Mshindi wa medali ya fedha ya Mashindano ya Afrika 2024, Kelvin Kipkorir, amesema analenga kushusha muda wake wa mita 400 hadi sekunde 43 mapema mwaka huu anapolenga kujumuishwa katika kikosi cha Kenya cha World Relays.
Mwanariadha huyo wa Kenya Prisons kwa sasa ana rekodi binafsi ya sekunde 44.80, aliyoiweka katika Mashindano ya Kitaifa mwaka jana alipomaliza wa tatu.
Mafanikio hayo yalikuwa hatua muhimu katika taaluma yake, yakimfungulia mlango wa kushiriki kwa mara ya kwanza Mashindano ya Dunia ya Riadha yaliyofanyika Tokyo.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 










































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































