IEBC YAZINDUA MPANGO WA USAJILI WA WAPIGA KURA KIDIJITALI
Tume Huru ya Uchaguzi na Mipaka (IEBC) imetangaza mpango wa kuzindua jukwaa la kidijitali litakalorahisisha zoezi la usajili wa wapiga kura, hasa kwa vijana.
Mwenyekiti wa IEBC Erastus Ethekon amesema jukwaa hilo litaruhusu wanaojiandikisha kujaza taarifa zao mtandaoni kabla ya kufika vituo vya usajili kuweka alama za kibayometriki.
Ethekon ame ongeza kuwa maandalizi ya Uchaguzi Mkuu wa 2027 yako kwenye mstari sahihi, huku usajili wa wapiga kura ukiwa ajenda muhimu ya tume ili kuongeza idadi ya Wakenya watakaoshiriki katika uchaguzi.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































