SHUMAH ANG’ARA LIGI KUU ZAMBIA
Mshambuliaji wa Kenya Moses Shumah anaendelea kung’ara katika msimu wa 2025/2026 akiwa na klabu ya Power Dynamos FC ya Zambia, akijidhihirisha kama mmoja wa washambuliaji tegemeo kuelekea mashindano ya AFCON 2027.
Mchezaji huyo wa zamani wa Kakamega Homeboyz anaongoza orodha ya wafungaji katika MTN Super League ya Zambia akiwa na mabao 12 tangu ajiunge na klabu hiyo Julai 2025.
Shumah alionyesha kiwango cha juu Machi 8 baada ya kufunga mabao matatu katika ushindi wa mabao 3–2 dhidi ya mahasimu wao Zesco United, matokeo yaliyomuweka kileleni katika kinyang’anyiro cha kiatu cha dhahabu.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































