RAIS RUTO AMEANZA ZIARA YAKE YA SIKU TATU KAUNTI YA NAKURU
Rais William Ruto ameanza ziara ya siku tatu katika kaunti ya Nakuru, akiwa na lengo la kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo ujenzi wa barabara ya Kinamba kuelekea Mengich, Murionduko na Kuresoi kaskazini .
Miradi hiyo inaolenga kuboresha miundombinu na kuimarisha uchumi wa eneo hilo.
Aidha, ameongoza shughuli ya upanzi wa miche elfu tano katika msitu wa mau, kama sehemu ya juhudi za serikali za kuhifadhi mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi.
Ziara hiyo inatarajiwa kuendelea kwa siku tatu, ambapo miradi mingine ya maendeleo inatarajiwa kuzinduliwa katika maeneo mbalimbali ya kaunti ya Nakuru.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































