NAIROBI YAONGOZA KWA MAAMBUKIZI YA UKIMWI
Kaunti ya Nairobi ndiyo inayoongoza kwa maambukizi ya ugonjwa wa UKIMWI, maambukizi mapya yakiongezeka kwa asilimia 19, ambayo ni sawa na watu 19,991 katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Haya ni kwa mujibu wa takwimu za kituo cha kudhibiti magongwa cha NSDCC, zikionyesha kuwa asilimia 60 ya mamabukizi mapya yalirekodiwa katika kaunti 10 ambazo ni Nairobi, Migori, Kisumu, Homa Bay, Busia, Siaya, Kakamega, Nakuru, Mombasa, na Bungoma.
Akizungumza kwenye hafla ya kuadhimisha siku ya UKIMWI duniani, mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi ameeleza haja ya kukabili maambukizi hayo hasa miongoni mwa Watoto na vijana.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 











































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































