#Local News

URUSI YAKANA KUWASAFIRISHA WAKENYA VITANI

Ubalozi wa Urusi humu nchini umejitenga na ripoti ya uchunguzi wa idara ya ujasusi NIS na ile ya upelelezi wa jinai DCI iliyouhusisha ubaliozi huo na madai ya kuwasafirisha wakenya kisiri kupigana katika vita kati ya Urusi na Ukraine.

Kupitia taarifa, ubalozi huo umesema kuwa ripoti hiyo si ya kweli, na kwamba haujakuwa ukitoa stakabadhi za usafiri kwa wakenya kusafiri nchini Urusi ili kushiriki vita hivyo.

Nazo familia za wakenya waliokwama vitani humo wametaka usaidizi wa kuwarejesha nchini jamaa zao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

URUSI YAKANA KUWASAFIRISHA WAKENYA VITANI

CHARLES KANJAMA RAIS MPYA LSK

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *