#Local News

MUDAVADI ATETEA FAMILIA YA RUTO

Mkuu wa mawaziri Musalia Mudavadi ambaye pia ni Waziri wa masuala ya kigeni, ameitetea familia ya Rais William Ruto dhidi ya madai kwamba inanufaika na biashara ya ulanguzi wa wakenya wanaoteseka katika mataifa ya Uarabuni jinsi ilivyoripotiwa na shirika la habari la New York Times.

Kwa mujibu wa shirika hilo, viongozi wakuu serikalini na familia yar ais Ruto ndio washikadau wakubwa katika kampuni zinazotoa huduma za bima kwa wakenya wanaosafirishwa katika mataifa hayo, likiongeza kuwa akina mama wanaojifungua nchini humo nje ya ndoa huteswa na kunyimwa huduma muhimu.

Hata hivyo akiwa mbele ya bunge la kitaifa, Mudavadi amekanusha madai hayo.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

MUDAVADI ATETEA FAMILIA YA RUTO

IEBC YAPOKEA VIFAA VYA CHAGUZI NDOGO

MUDAVADI ATETEA FAMILIA YA RUTO

RUTO KUHUTUBIA TAIFA BUNGENI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *