OMTATAH MAHAKAMANI KUPINGA KITUO CHA IEBC
Seneta wa Busia Okiya Omtatah amewasilisha kesi mahakamani akitanga mahakama itoe agizo kwamba tume huru ya uchaguzi na mipaka IEBC imekuwa ikikiuka katiba kwa kuanzisha na kuendesha kituo cha kitaifa cha kujumlisha kura, chenye uwezo wa kuhakiki, kubadilisha au kujumlisha upya matokeo ya urais.
Kwenye kesi yake, Omtatah amekariri vipengee vya 86 na 138 vya katiba, inavyokariri kuwa matokeo yanayotangazwa katika maeneo bunge ndiyo ya mwisho na hayawezi kubadilishwa.
Amesisitiza kuwa kipengee cha 39 cha sheria za uchaguzi kilichozindua kituo hicho, kinakiuka katiba.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 


















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































