MAKALI AOMBA SUBIRA KWA WAFANYAKAZI WA SUKARI
Mbunge wa Kanduyi John Makali amewaomba wafanyakazi wa viwanda vya sukari katika mkoa wa Magharibi kuwa na subira huku serikali ikiendelea kushughulikia ulipaji wa malimbikizi ya mishahara yao.
Akizungumza katika kaunti ya Bungoma, Makali ametoa hakikisho kuwa serikali iko mbioni kuhakikisha wafanyakazi pamoja na wakulima wa miwa wanalipwa fedha wanazodai kwa wakati unaofaa.
Hata hivyo, amewasuta baadhi ya watu anaodai wanatumia suala hilo kuchochea vurugu na maandamano, akisema hatua kama hizo haziwezi kusaidia kutatua changamoto zinazokumba sekta ya sukari.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































