KENYA YATEULIWA KUWA MWENYEJI HSBC
Shirikisho la raga ulimwenguni limethibitisha kwamba Kenya itakuwa mwenyeji wa mechi za ufunguzi za HSBC SVNS 2, likiwa tukio la kihistoria kwa Kenya na ukanda wa Afrika Mashariki.
Kipute hicho kitakachosakatwa tarehe 14 na 15 Februari mwaka ujao jijini Nairobi kitapisha dimba la kimataifa la Sevens Circuit, ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nchini Kenya.
Kenya itakuwa mwenyeji wa mikondo 3, huku Brazil na Uruguay wakiwa wenyeji wa mikondo inayofuata.
Dimba hilo litahusisha timu mbali mbali za wanawake na wanaume.
Katika kipute cha wanaume, Kenya itamenyana na USA, Germany na Uruguay katika usakaji wa tiketi ya kupandishwa daraja.
Katika kitengo cha wanawake, Kenya Lionesses watamenyana na Brazil, Uhispania na Uchina.
Dimba hilo limepewa jina rasmi la HSBC Nairobi Sevens.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 

























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































