AJALI YA BODA BODA YAUA MWANAMKE BUSIA
Mwanamke mwenye umri wa makamo ameaga dunia kufuatia ajali ya barabarani iliyohusisha boda boda katika eneo la Mlango Kumi, kwenye barabara kuu ya Busia kuelekea Kisumu.
Ajali hiyo ilitokea mapema hii leo, huku chanzo chake kikisalia kutambuliwa na maafisa wa polisi waliowasili eneo la tukio kufanya uchunguzi.
Abiria wengine wawili waliojeruhiwa katika ajali hiyo walikimbizwa katika hospitali ya kibinafsi Bulanda, Kaunti ya Busia, kwa matibabu ya dharura.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 







































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































