BARCELONA YAMSAJILI CHIPUKIZI AJAY TAVARES
Klabu ya FC Barcelona imemsajili mchezaji chipukizi Ajay Tavares kutoka akademi ya Norwich City.
Tavares, mwenye umri wa miaka 16, anaripotiwa kuvutia vilabu kadhaa barani Ulaya. Norwich itapokea fidia ya malezi, ingawa haijathibitisha kiasi cha fedha kinachohusika katika makubaliano hayo.
Mchezaji huyo alijiunga na Norwich akiwa chini ya umri wa miaka 12. Msimu uliopita alitokea benchi katika mechi ya kirafiki ya kujiandaa na msimu mpya dhidi ya klabu ya Uholanzi, FC Volendam, akiwa na umri wa miaka 15.
Imetayarishwa na Cyrus Sifuna
English 




























































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































