ARSENAL WADUMISHA REKODI UEFA
Noni Madueke alifunga mara 2 klabu yake ya Arsenal ilipopata ushindi wa magoli 3-0 ugenini dhidi ya Club Brugge, na kudumisha rekodi yao ya kutopoteza mechi katika ligi ya klabu bingwa bara Ulaya msimu huu.
Arsenal sasa ndio timu ya pekee ambayo imefuzu awamu ya mwondoano kutokana na ushindi huo, ikiwa na pointi 18 katika mech izote 6.
Kocha Mikel Arteta alifanya mabadiliko kwenye kikosi kilichopoteza wikendi dhidi ya Aston Villa, na kuwaleta wachezaji wapya akiwemo Madueke aliyefungua ufungaji kabla ya Gabriel Martinelli kufunga bao la 3.
Kwenye pambano hilo, Arsenalpia walikaribisha kurejea kwa Gabriel Jesus baada ya kukaa nje kwa siku 342 kutokana na jeraha, huku Kinda Marli Salmon mwenye umri wa miaka 16 akijumuishwa kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































