ATLETICO MADRID WANUSIA UBINGWA WA COPA DEL REY
Mabao ya Ademola Lookman, Antoine Griezman na Julian Alvarez yaliwapa Atletico Madrid ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Barcelona katik a mkondo wa kwanza wa nusu fainali ya dimba la Copa del Rey, na kuwapa harufu ya ubingwa wa taji hilo wanapojiandaa kusaka tiketi ya kuingia fainali watakapovaana kwa mkondo wa pili.
Masaibu ya Barca yalianza wakati Eric Garcia alijifunga bao kunako dakika ya 7, kabla ya kichapo kufuata, Atletico wakitekeleza maangamizi katika kipindi cha kwanza.
Mechi ya mkondo wa pili itachezwa Nou Camp tarehe 3 mwezi ujao.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 














































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































