SERIKALI HUZIMA UMEME, RUTO
Umeme ambao umekuwa ukipotea katika baadhi ya maeneo nchini kati ya saa kumi na moja jioni na saa nne usiku umekuwa ukizimwa na serikali kutokana na mahitaji ya juu ya umeme ambayo serikali haiwezi kutosheleza.
Haya ni kwa mujibu wa rais William Ruto kwenye kikao na wakenya wanaoishi nchini Qatar, akisema Kenya inahitaji zaidi ya shilingi trilioni 1 kuongeza umeme utakaotosha mahitaji hayo.
Aidha, amewahimiza wakenya kuchangia maendeleo ya taifa bila serikali kuchukua madeni ya kigeni.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 












































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































