#Business

SACCOS 116 ZAPOKEA FIDIA BAADA YA KASHFA YA KSH 13B KUSCCO

Muungano wa Vyama vya Ushirika vya Akiba na Mikopo nchini (KUSCCO) umelipa Ksh152.4 milioni kwa SACCOs 116 na wawekezaji binafsi, na hivyo kuashiria hatua nyingine katika mpango wake wa urejeshaji kufuatia kashfa ya kifedha ya Ksh13.3 bilioni iliyofichuliwa mapema mwaka huu.

Kama ilivyoripotiwa ni kwamba, fidia ya hivi punde imeleta jumla ya malipo hadi Ksh369.3 milioni, na kuongeza kwa Ksh216.9 milioni zilizosambazwa mwaka jana.hata hivyo imebainika kuwa SACCOs zilikuwa zimewekeza mabilioni katika KUSCCO, lakini ukaguzi wa kitaalamu ulifichua hasara kubwa iliyohusishwa na maafisa wa zamani, ambao tangu wakati huo wameshtakiwa mahakamani.

KUSCCO sasa inalenga urejeshaji wa angalau 70% ya kampuni kuu ya Ksh8.8 bilioni iliyowekezwa na SACCOs ndani ya miaka mitatu, kwa kutumia mapato ya mauzo ya mali, minada na urejeshaji wa mikopo.

Imetayarishwa na Maureen Amwayi

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *