UKATILI WA MAFURIKO TRANS NZOIA
Zaidi ya familia 3,000 katika maeneo ya Namanjalala na Kapomboi kaunti ya Trans Nzoia zinalilia msaada wa dharura kutokana na mafuriko baada ya mto Sabwani kuvunja kingo zake na kuwaacha bila makao.
Mafuriko hayo yamesomba mashamba na makazi, waathiriwa wakikabiliwa na athari za magonjwa mbali na hasara kutokana na uharibu wa mazao yao.
Waathiriwa wamehimiza ushirikiano wa serikali kuu na ile ya kaunti kutatua changamoto hizo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 





















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































