#Local News

HOFU YA USALAMA WA RAIS RUTO

Hofu imeibuka kuhusiana na usalama wa Rais William Ruto hasa kutokana na majaribio ya raia kumrukia akiwa majukwaani, tukio la hivi punde likiwa hapo jana ambapo Rais Ruto aliokolewa na walinzi kwenye jukwaa dhidi ya kukabiliwa na jamaa mmoja katika kaunti ya Wajir.

Hatua hiyo ilimlazimu Rais kusitisha hotuba yake na kuangazia tukio hilo, ambalo limeibua hofu hasa baada ya tukio sawa katika kaunti ya Mombasa wiki jana wakati wa hafla ya usambazaji wa fedha za NYOTA, kijana aliyejaribu kumkimbilia jukwaani akikiri kumwandama katika hafla kadhaa.

Tishio jingine la kiusalama dhidi ya Rais lilishuhudiwa mwaka jana katika kaunti ya Migori baada ya raia mmoja kumlenga na kiatu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

HOFU YA USALAMA WA RAIS RUTO

ODM: MPASUKO WETU UNATOKA NJE YA CHAMA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *