#Local News

SIFUNA ASISITIZA ODM INGALI AZIMIO

Katibu mkuu wa chama cha ODM Edwin Sifuna, amesisitiza kwamba chama hicho kingali mwanachama wa muungano wa Azimio la Umoja One Kenya, na kwamba anawaunga mkono viongozi wapya walioteuliwa kuongoza muungano huo mapema wiki hii.

Kwenye mahojiano na kituo kimoja cha runinga, Sifuna amekariri hitaji la sheria linaloitaka ODM kuwasilisha notisi ya siku 90 kwa msajili wa vyama vya kisiasa kuhusu azma yake ya kuondoka.

Katika mageuzi mapya, Kalonzo Musyoka ameteuliwa kuwa kinara mpya wa Azimio kuchukua mahali pa marehemu Raila Odinga, huku mbunge wa Suba North Karoli Omondi akichukua mahala pa Junet Mohammed kama katibu mkuu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

SIFUNA ASISITIZA ODM INGALI AZIMIO

IEC MBIONI KUJAZA PENGO LA MARIJAN

SIFUNA ASISITIZA ODM INGALI AZIMIO

BUSIA KWENYE DARUBINI YA EACC

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *