#Local News

ODM YAPINGA MAGEUZI YA UONGOZI AZIMIO

Mageuzi ya hivi punde ya uongozi katika muungano wa Azimio yameendelea kuibua mvutano kwenye muungano huo, chama cha ODM sasa kikiyapuzilia mbali kwa misingi kwamba kinara wake Oburu Oginga hakushirikishwa wala kuhusishwa.

Kulingana na ODM, mabadiliko hayo yaliyotangazwa na Rais Mstaafu Uhuru Kenyatta, ni batili na kinyume na sheria za muungano huo, ikimtaka msajili wa vyama vya kisiasa John Lurionokou kusitisha utekelezaji wa mabadiliko hayo.

Miongoni mwa pingamizi ni uteuzi wa Kalonzo Musyoka kuwa kinara wa Azimio, ODM ikisisitiza kuwa mageuzi hayo yanafaa kufanywa na vyama tanzu.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

ODM YAPINGA MAGEUZI YA UONGOZI AZIMIO

RUTO ATETEA MIRADI YAKE

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *