#Football #Sports

UEFA YAIDHINISHA CAMP NOU KLABU BINGWA INAPOREJEA

Shirikisho la soka barani Ulaya UEFA limeiruhusu klabu ya Barcelona kuchezea mechi zake za klabu bingwa barani Ulaya kwenye uwanja wa nyumbani wa klabu hiyo Camp Nou.

Kupitia taarifa, miamba hao wa La Liga wamesema UEFA imeidhinisha ombi lao kwa kuzingatia kuwa mahitaji muhimu yameafikiwa.

Barcelona ambao wamekuwa wakichezea katika viwanja mbali mbali kwa miaka 2 kutokana na ukarabati wa Camp Nou, watakuwa wenyeji wa Eintracht Frankfurt uwanjani humo tarehe 9 Disemba, wiki 2 baada ya kuuzindua dhidi ya Athletic Bilbao katika mechi ya la Liga Jumamosi hii.

Kutokana na kucheleweshwa kwa ufunguzi wa uwanja huo, Barca walilazimika kuchezea katika uwanja wao wa mazoezi wenye uwezo wa kuwabeba mashabiki 6,000 pekee katika wiki za kwanza za msimu baada ya kukosa kupata leseni ya kuuzindua uwanja wao.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *