#Local News

POLISI NA NCIC WACHUNGUZA KESI 12 ZA CHUKI NA UCHOCHEZI

Huduma ya Kitaifa ya Polisi kwa ushirikiano na Tume ya Kitaifa ya Uwiano na Utangamano (NCIC) zimechunguza kesi 12 za matamshi ya chuki, uchochezi wa vurugu, unyanyasaji mtandaoni na usambazaji wa maudhui ya uchochezi katika kipindi cha mwaka mmoja uliopita.

Akizungumza mbele ya Kamati ya Kudumu ya Seneti kuhusu Uwiano wa Kitaifa, Fursa Sawa na Ujumuishaji wa Kieneo, Inspekta Jenerali wa Polisi Douglas Kanja amesema kesi nyingi bado zinaendelea kuchunguzwa huku chache zikiwa zimepiga hatua katika mchakato wa kisheria.

Kanja ameonya kuwa akaunti za mitandao ya kijamii zinazoendeshwa kutoka nje ya nchi pamoja na majukwaa ya mawasiliano yaliyosimbwa kwa siri vinatatiza juhudi za kudhibiti matamshi ya chuki na uchochezi, hasa pale maudhui yanapotoka nje ya mamlaka ya Kenya au kutumwa bila kutambulika mhusika.

Imetayarishwa na Cyrus Sifuna

POLISI NA NCIC WACHUNGUZA KESI 12 ZA CHUKI NA UCHOCHEZI

UWEKAJI MSINGI WA UPANUZI WA SGR HADI

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *