#Football #Sports

KOMBE LA DUNIA: DR CONGO YAWEKA HAI MATUMAINI

Timu ya taifa ya soka ya DR Congo iliweka hai matumaini ya kushiriki mtanange wa kombe la dunia mwaka ujao baada ya kuwakata kucha Super Eagles wa Nigeria katika fainali za mwondoano wa shirikisho la soka barani Afrika CAF jana usiku nchini Morocco.

Leopards, jinsi wanavyofahamika walizima ndoto ya Nigeria kwa kuwalaza mabao 4-3 kupitia mikwaju ya penalti, baada ya muda wa kawaida na ziada kutamatika kwa sare ya goli 1.

Wing’a wa Lille Chancel Mbemba, alifunga mkwaju wa ushindi katika makabiliano yaliyoshuhudia mikwaju 4 ikipanguliwa, kipa wa DR Congo Timothy Fayulu aliyechukua nafasi ya mwenzake Lionel Mpasi dakika za mwisho, akipangua mara 2.

DR Congo watasaka tiketi ya kucheza kombe la dunia, watakaposhiriki mwondoano wa mwisho wa mabara mwezi Machi mwaka ujao nchini Mexico, watakapombana na timu zaidi kutoka Bara Asia, Marekani na Oceania, na iwapo watafanikiwa, bara la Afrika litawakilishwa na mataifa 10 katika kipute hicho.

Mara ya mwanzo na mwisho kwao kushiriki kombe la dunia ulikuwa mwaka wa 1974, wakati huo wakiitwa Zaire na ni tukio ambalo hawapendi kukumbuka ikizingatiwa kuwa walifungwa mabao 14 bila jibu, ikiwemo 9-0 dhidi ya Yugoslavia katika awamu ya makundi.

Imetayarishwa na Antony Nyongesa

KOMBE LA DUNIA: DR CONGO YAWEKA HAI MATUMAINI

HOMEBOYZ WASHINDWA KUREJEA ‘NYUMBANI’

KOMBE LA DUNIA: DR CONGO YAWEKA HAI MATUMAINI

HAALAND AIREJESHA NORWAY KOMBE DUNIA

Leave a comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *