SHERIA YAWAGAWANYA WABUNGE
Wabunge wamechukua misimamo kinzani kuhusiana na sheria ya kuanzishwa kwa hazina ya kitaifa ya miundombinu inayopendekezwa ya mwaka 2025 kwa lengo la kuanzisha hazina ya kufadhili miradi mikubwa iliyoidhinishwa na baraza la mawaziri kama sehemu ya kuokoa uchumi.
Wabunge wa upande wa serikali akiwemo Owen Baya wa Kilifi North na Silvanus Osoro wa South Mugirango, wametetea sheria hiyo wakisema kuanzishwa kwa hazina hiyo kutaimarisha ujenzi wa miundombinu nchini.
Hata hivyo, wenzao wa upinzani akiwemo Makali Mulu wa Kitui Central, Oundo Mudenyo wa Funyula na Caroli Omondi wa Suba South, wameibua hofu kuhusu uhalali wa hazina hiyo.
Imetayarishwa na Antony Nyongesa
English 



















































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































































